QNET, kampuni ya kimataifa ya mtindo wa maisha na ustawi, imepata kutambuliwa kimataifa kwa msimamo wake thabiti dhidi ya udanganyifu. Kampeni ya kampuni hiyo iitwayo QNET Against Scams imetunukiwa Tuzo ya Dhahabu ya Stevie® katika hafla ya 22 ya International Business Awards (IBA), ikionyesha kujitolea kwa QNET kulinda wateja na kudumisha uadilifu wa chapa yake.
Kutambuliwa katika International Business Awards
Katika Tuzo za IBA za 2025, QNET ilipokea:
- Tuzo ya Fedha ya Stevie® kwa kampeni hiyo hiyo katika kipengele cha Public Service.
- Tuzo ya Dhahabu ya Stevie® kwa kampeni ya QNET Against Scams: Rebuilding Trust Through Crisis Communication and Public Education in Ghana katika kipengele cha Communications or PR Campaign of the Year – Brand / Reputation Management.
- Tuzo ya Shaba ya Stevie® kwa V-Africa 2025: Rebuilding Trust and Empowering Entrepreneurs in Africa Through QNET’s Flagship Convention katika kipengele cha Corporate & Community – Community Engagement Event.
Heshima hizi zimeiweka QNET miongoni mwa chapa zinazoongoza duniani zinazotambulika kwa ubora katika mawasiliano na uwajibikaji wa kijamii wa kampuni.
Kuhusu Kampeni ya QNET Against Scams
Kampeni hii ilizinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Ghana mwaka 2024, kisha ikapanuliwa hadi Senegal na Sierra Leone. Lengo lake kuu ni kupambana na matumizi mabaya ya jina la QNET na wadanganyifu, na kuelimisha jamii jinsi ya kutofautisha biashara halali ya direct selling na ulaghai. Kampeni hii ilijumuisha mabango barabarani, matangazo ya redio na televisheni, vipeperushi vya michoro, mitandao ya kijamii, na mashughuli za uhamasishaji mitaani — ikiwemo timu za wa-sketa — huku ikishirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama na wadhibiti ili kuimarisha ulinzi wa watumiaji.
Umuhimu wa Kampeni ya Kupinga Ulaghai ya QNET
Watu wasio waaminifu wamekuwa wakidanganya jamii kwa kutumia jina la QNET kwa uwongo, wakiahidi ajira, viza, au faida za haraka. Kampeni hii imeweka wazi kuwa QNET ni kampuni ya mauzo ya moja kwa moja (direct selling), na mapato hupatikana tu kupitia mauzo ya bidhaa zake za ustawi na mtindo wa maisha, ikionya umma kuwa makini dhidi ya madai ya uongo yanayotolewa kwa jina lake.
Athari za Kampeni
- Ufikaji wa Jamii: Maelfu ya watu walihusishwa kupitia matukio ya jamii na shughuli za uhamasishaji katika miji mikuu.
- Ushirikiano: Ushirikiano na taasisi kama Ghana’s Economic and Organised Crime Office (EOCO), Ghana Police Service, Immigration Service, na Nigeria’s EFCC.
- Zana za Uwazi: Uzinduzi wa tovuti maalum ya Scam Alert kusaidia watumiaji kutambua na kuripoti ulaghai.
- Ushirikiano na Vyombo vya Habari: Upeo mkubwa wa habari kupitia mikutano ya waandishi wa habari na juhudi za kuhakikisha utiifu wa sheria.
Kwa mujibu wa ripoti ya 2024 Global State of Scams iliyotolewa na Global Anti-Scam Alliance (GASA) na Feedzai, hasara za kimataifa kutokana na ulaghai zinakadiriwa kufikia dola za Marekani trilioni 1.03 katika miezi 12 iliyopita — jambo linaloonyesha umuhimu wa ulinzi wa watumiaji unaoongozwa na mashirika.
Maana ya Ushindi Huu kwa QNET
Tuzo hizi ni uthibitisho wa juhudi zetu katika kupambana na wale wanaotumia vibaya jina letu kudanganya wengine. Tumejizatiti kulinda jamii tunazohudumia na kujenga upya imani kati yetu na wateja pamoja na wadau wetu. Pamoja, tuzo hizi zinathibitisha dhamira yetu kwa uanzishaji wa biashara zenye uwajibikaji na maadili yanayotusukuma mbele.” — Trevor Kuna, Afisa Mkuu wa Masoko wa QNET