Orodha hii ni kwa ajili yako wewe uliye weka mipango ya safari mwaka huu lakini kutokana na vizuizi vya Covid-19. Ulimwengu unapoendelea kuimarika, unaweza kujikuta unaweza tu kusafiri ndani ya nchi. Bado unaweza kuendelea kufurahia safari zako kwa kuunda orodha ya vitu vinavyoweza kutekelezeka ili kuifanya likizo yako kuwa ya kipekee na ya kukumbukwa zaidi. Haya hapa ni mawazo machache ya safari yako ijayo.
1. Tazama mawio na machweo ya jua siku hiyo hiyo
Tunakumbuka sikukuu kwa furaha kwa sababu ni wakati katika maisha yetu tunapopunguza mwendo na kufurahia maisha kikweli. Ili kufanya likizo yako ijayo ikumbukwe, amka mapema ili ushuhudie mawio na utazame machweo ya jua siku hiyo hiyo. Piga picha ukitaka, lakini furahiya kwa kutazama tu anga ikibadilisha rangi.
2. Jifunze kupika chakula kutoka nchi geni
Njia bora ya kujishughulisha na likizo ni kujaribu na kujifunza kitu kuhusu eneo unalotembelea. Na njia bora ya kujifunza kuhusu watu ni kujifunza kuhusu chakula wanachopenda. Jiandikishe katika kozi ili ujifunze jinsi ya kupika chakula chao. Ikiwa hupendi kupika, tafuta mama au kisoki kidogo na kula huko badala ya mgahawa mkubwa.
3. Nenda kwenye matukio ya jumuiya
Mojawapo matarajio/ndoto zinazoweza kufikiwa ni kuhudhuria kitu cha jumuiya – soko ndogo, onyesho dogo la bendi ya mtaani, tamasha la jumuiya. Kuelewa mahali unapotembelea kupitia macho ya matukio ya kila siku kama hayo kutakufanya uthamini likizo yako zaidi.
4. Jaribu kitu kipya kitachokuogopesha
Ikiwa kukaa kimya na kuwepo katika uhalisia kunakuogopesha, basi simama na unuse maua/waridi. Ikiwa kuwa mbali na simu yako kunakuogopesha, basi fanya mapumziko mafupi ya mitandao ya kijamii kwa saa kadhaa. Ongea na mgeni na ufanye marafiki. Chochote kinachokuogopesha, jiwekee changamoto na ukikamilishe.
5. Jipe vitu vyenye thamani
Miaka miwili iliyopita imekua migumu na unastahili angalau usiku kadhaa katika mapumziko ya likizo iliyoratibiwa haswa kwa ajili yako. Jivinjari kwa kuchagua likizo kwenye QVI, iwe unatafuta mapumziko mafupi au ya muda mrefu zaidi, utapata kitu cha kujifurahisha nacho.
6. Jitafutie Zawadi ya ukumbusho
Hili ni jambo zuri unaloweza kufanikisha – Jinunulie zawadi ambayo itakukumbusha likizo yako. Utachangia uchumi wa ndani na kuchukua kitu kinachoonekana kukukumbusha likizo yako. Sio lazima kuwa mapambo ya jokofu,unaweza kuchagua kito kinyume na kile unachochagua mara kwa mara kama ukumbusho wako. Rudi na kikombe cha kahawa ili ujikumbushie likizo yako au labda kipande kidogo cha vito. Chaguo ni lako.
7. Jitolea katika shirika la usaidizi la ndani
Kama balozi wa RYTHM popote unapoenda, ni vizuri kufanya mabadiliko katika maeneo unayotembelea. Jitolee kwenye makazi ya wanyama au jikoni. Tumia muda wako na watu wasiojiweza na kuleta tabasamu kwenye nyuso zao. Sio tu kwamba hiki ni sehemu ya orodha ya vitu vya kufnaikisha, pia inamaanisha unaacha athari kubwa bila juhudi nyingi kutoka kwako. Nafasi yoyote ya Kujiinua Kusaidia Wanadamu ni nafasi ambayo tunapaswa kuchukua.
Matamanio ya vitu vya kufanya kablda ya kuondoka duniani, ni orodha inakusudiwa kuwa orodha ya mambo unayotaka kufikia kabla ya kufariki. Kawaida hujazwa mara moja katika maisha. Lakini kwa kuwa ulimwengu na likizo ndivyo zilivyo, tumeipunguza kwa vitu hivi vinavyoweza kufikiwa na bado vya kusisimua. Je, ni kipi kati ya vitu hivi utajaribu kwenye likizo yako ijayo? Tujulishe kwenye maoni.