Tuzo za World CEO za 2021 zilimtambua Mkurugenzi Mtendaji wa QNET Malou Caluza kwa kumpatia tuzo ya Gold Globee®. Bi Malou Alitalia kua Mkurugenzi Mtendaji Mwanamke wa Mwaka katika Kitengo cha Bidhaa za Watumiaji katika toleo la 9 la mwaka la shindano hili. Mkurugenzi Mtendaji wa QNET Malou Caluza sio tu mtetezi wazi wa wanawake katika biashara na uongozi, lakini pia ni mkongwe wa mauzo ya moja kwa moja ambaye amewahamasisha mamilioni. Hii ni tuzo inahistahili sana kama mwanamke ambaye amejitolea maisha yake kwa huduma.
Tuzo za Dunia za Wakurugenzi Watendaji wa 2021
Katika mwaka wake wa 9, Tuzo za Dunia za wakurugenzj ziliundwa ili kuwaenzi Wakurugenzi Wakuu, wasimamizi, wajasiriamali na wabunifu kutoka kote ulimwenguni. Tuzo hizi zinatambua mafanikio na michango ya walio bora zaidi katika uongozi na uwajibikaji wa kijamii. Tuzo hizo ni sehemu ya mashindano kumi na moja chini ya mwamvuli wa Tuzo za Globee, zikiwemo Tuzo za Kimataifa za Biashara Bora Zaidi na Tuzo za Golden Bridge ambazo QNET ilishinda mapema mwaka huu. Mkurugenzi Mtendaji wa Kike wa Mwaka hutunukiwa kwa watu ambao wameweka alama za juu katika tasnia kwa ubora. Hatuwezi kufikiria mtu anayestahiki zaidi sifa hii kuliko Mkurugenzi Mtendaji wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa QNET Malou Caluza
Bi Malou anaongeza Gold Globee® kwenye orodha yake ya mafanikio, ikiwa ni pamoja na ushindi wake dhidi ya saratani ya matiti. Pia aliangaziwa katika chapisho la “Asia’s 15 Over 50” linaloadhimisha wanawake waliofanikiwa zaidi barani Asia. Bi Malou ni msukumo kwa wajasiriamali wote, baada ya kunyanyuka hadi cheo cha Mkurugenzi Mtendaji baada ya kuanza kama Afisa wa Huduma kwa Wateja QNET.
“Ni heshima kutambuliwa na Tuzo za Dunia za Wakurugenzi Watendaji wa 2021 na Gold Globee – Ninashukuru sana timu yangu ya QNET kwa bidii yao isiyoyumba na bidii ambayo, kwa upande wake, imenisukuma kuwa kiongozi bora kila siku,” alisema Bi Malou. “Tunaamini kuwa utambuzi huu kutoka kwa Tuzo za Globee zinathibitisha zaidi kujitolea kwetu kuwawezesha wajasiriamali wengi zaidi na bidii yetu ya kuendelea kuwazingatia wateja.”
Ungana nasi kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wetu wa QNET, Malou Caluza kwa mafanikio haya mazuri. Shiriki habari na familia yako ya QNET au acha maoni yako hapa chini.