Je, Uko Tayari Kuanza Safari Yako kama Msambazaji Huru wa QNET (ID)? Huo ni uamuzi mzuri sana! Mchakato wa kujisajili na QNET ni rahisi, na tuko hapa kukuongoza hatua kwa hatua. Fuata tu maelekezo hapa chini, na kwan muda si mrefu utakuwa tayari kuanzisha biashara yako!
Usajili wa QNET | Jinsi ya Kujiunga na QNET
Kujisajili Kupitia Tovuti ya QNET
Hatua ya 1: Tembelea Tovuti ya QNET
Kwanza, nenda kwenye www.qnet.net. Tafuta alama ya mtumiaji iliyo juu kulia ya skrini yako. Bofya hapo, na utakuwa umeanza safari yako!
Hatua ya 2: Jaza Taarifa Zako Binafsi
Utaombwa kutoa Nambari ya Msambazaji wa Mrejeleo wako (Referrer’s ID) na nchi unakotaka kusajiliwa. Ukishamaliza, utapelekwa kwenye ukurasa wa kujaza taarifa zako binafsi kama jina lako, barua pepe, nambari ya simu, na anwani ya nyumbani. Utahitajika pia kuunda nywila (password) na kuchagua mpangilio wako (placement).
Baada ya hapo, ujumbe wa kuthibitisha (OTP) utatumwa kwenye simu yako. Ingiza OTP hiyo ili kuthibitisha nambari yako ya simu — na utakuwa tayari kuendelea!
Hatua ya 3: Kubali Sheria na Masharti
Kabla ya kukamilisha usajili wako, chukua muda kusoma na kukubali Sera na Taratibu za QNET, Kanuni za Maadili, na Taarifa ya Mapato na Faida. Hati hizi ni muhimu kwani zinaeleza wajibu wako kama Msambazaji Huru na jinsi biashara inavyofanya kazi.
Hatua ya 4: Lipa na Thibitisha Usajili Wako
Hatimaye, chagua kifurushi cha usajili unachotaka na endelea na malipo. Mara tu malipo yako yatakapokamilika, utapokea risiti ya uthibitisho pamoja na Nambari yako mpya ya Msambazaji (ID).
Angalia mwongozo kamili wa usajili kwa maelekezo zaidi.
Kujisajili Kupitia App ya Simu ya QNET
Hatua ni zile zile — unazifanya tu kupitia app! Jifunze zaidi kuhusu QNET Mobile App iliyoshinda tuzo hapa.
Haijalishi umechagua njia gani ya kujisajili, mchakato ni rahisi sana. Fuata tu hatua hizi rahisi — na huo ndio mwanzo wa safari yako! Sasa umefanikiwa kuwa Msambazaji Huru wa QNET rasmi.