Heri ya Mwaka wa Chui 2022 nyote! Tunapoadhimisha Mwaka Mpya wa Lunar, hebu tuangalie kile mnyama Chui anaashiria na nini maana yake kwa wauzaji wa moja kwa moja na wajasiriamali.
Mwaka wa Chui ni nini?
Kulingana na usomaji nyota wa Kichina, kila mwaka mpya huleta mwanzo mpya unaopewa jina la moja ya wanyama wa nyota hizo. Mwaka huu, tunasherehekea Mwaka wa mnyama Chui , haswa wa majini. Miaka ya awali ya Chui ilikuwa 1974, 1986, 1998 na 2010. Chui anachukuliwa kuwa mfalme wa msitu katika nchi za Asia, na watu waliozaliwa chini ya ishara hii wanasemekana kuwa wakali vile vile. Ikiwa wewe ni Chui katika nyota za Kichina, unajulikana kwa ujasiri wako, ustadi na kua na imani kali za haki ya kijamii. Hata kama wewe sio Chui , kila mwaka wa Chui ni ishara ya matukio muhimu yatakayo badilisha maisha. Kwa hiyo, mwanzo wa mwaka mpya wa mwezi Februari 1, ni wakati wa kuwa waangalifu, lakini pia kufuata ndoto zako kubwa, na kuwa mthubutu.
Vidokezo kwa Wajasiriamali Katika Mwaka wa Chui
Iwe unaamini katika usomaji nyota au la, kuna masomo makubwa zaidi unayoweza kujifunza kutoka kwa Mwaka huu Mpya wa 2022. Haya ni baadhi ya viashirio vinavyohusiana na mwaka wa Chui ambayo unaweza kufanya.
Kuwa mwangalifu
Unapozingatia uhusiano mpya wa kifedha au hata gharama kubwa, kuwa mwangalifu. Mwaka huu, hakikisha unafanya utafiti wako kikamilifu na kuelewa athari zote za kifedha kabla ya kuchagua kujikita mzima mzima. Usirukie mradi kwa kutamani, lakini fanya kwa sababu umetumia muda kuufikiria. Zingatia afya yako, jitunze na ujiangalie. Kula vizuri, fanya mazoezi na ulinde afya yako ya akili. Na uwe #QNETPRO.
Kua na msukumo
Alama ya mwaka huu ni maji, ambayoo ni ishara ya ubunifu na msukumo. Mkumbatie mtu wako wa ndani na usiogope kushughulikia matatizo kwa njia yako ya kipekee. Fikiria nje ya boksi na uruhusu juisi za ubunifu zitirike. Onyesha shauku yako ya kuuza moja kwa moja kupitia vitendo vyako, na wacha wengine wahamasishwe. Kuwa mwenye kubadilika na kukumbatia/kupokea mabadiliko kama fursa ya kukuza mafanikio.
Uwe Mwenye Kutamani na Mtu wa uthubutu
Kuwa na malengo mwaka huu. Tumia vyema fursa ulizo nazo na ujifanyie kazi kwelikweli. Chukua kozi hiyo ambayo umekuwa ukitaka kusoma kila wakati. Badili taaluma na uanzishe biashara yako mwenyewe. Ongea na wale watu ambao uliogopa kuwakaribia. Huu ni mwaka wako wa kuwa na ujasiri. Weka malengo makubwa zaidi na ufanye mpango wa kuyafikia. Na usisahau kubadilika na kuwa wazi kuokea mabadiliko.
Jenga Timu Yako
Mwaka huu, onyesha upendo wako kwa njia tofauti. Tumia wakati mwingi na familia yako, waoigie simu time yako hila sababu, na ujihusishe katika shughuli zinazobadilisha na kuleta mabadiliko katika jumuiya kuifanya kuwa bora. Acha matendo yako yazungumze zaidi kuliko maneno yako. Tumia muda kuunda timu yako mwaka huu, na ufanye mazoezi ya RYTHM kila fursa unayopata.