Ramadhani mwaka 2022 ilikuwa ya ushindi kwani QNET iliendelea kuheshimu mila zetu kw akueneza maadili ya RYTHM. Mwezi mtukufu ulishuhudia shughuli nyingi kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya serikali na mashirika yasiyo ya faida duniani kote, kueneza upendo na amani kwa jamii zilizo hatarini zaidi na ambazo hazijhudumiwa. Huku jamii zikiendelea kupata nafuu kutokana na janga la kimataifa ambalo limekuwepo kwa zaidi ya miaka miwili, Ramadhani mwaka 2022 ilionekana kuwa fursa nzuri ya kutoa msaada. Tunaeneza furaha ya EID na msimu mtukufu kwa usaidizi wa IRs zetu za ajabu duniani kote, pamoja na wafanyakazi wetu waliojitolea. Hapa kuna mambo muhimu ziadi kutoka kwenye shughuli za mwezi mzima.
Kueneza Ramadhani katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
QNET ilitoa msaada wa chakula na vifaa vya choo nchini Tanzania. Hii pamoja na kutoa msaada wa fedha kwa kituo cha watoto yatima cha Mazizini Zanzibar, na kituo cha kulelea watoto yatima cha Chakuwama kilichopo Dar ees salaam.
Nchini Nigeria, shughuli za QNET za Ramadhani mwaka 2022 zilijumuisha kuchangia chakula na vitu muhimu kwa kituo cha watoto yatima cha Door of Peace, kituo ambacho kimekuwa na familia za waislamu walio katika mazingira magumu tangu mwaka 1990.
Chakula cha jioni cha iftari kiliandaliwa katika hospitali moja nchini Ghana, kwa usaidizi wa wafanyakazi wa QNET na wasambazaji huru. Iliuwa jioni ya chakula cha pamoja, hisia na vicheko vingi ambavyo vilimalizika kwa mchango wa ukarimu wa vitu muhimu kwa hospitali.
Ikifanya kazi na msikiti wa Abidjan,Ivory Coast, QNET ilianda iftari kwa kaya nyingi baada ya sala ya jioni.
Kusambaza furaha katika Mashariki ya Kati na Africa Kaskazini
QNET iliandaa futari na kutoa vitu muhimu katika jumuiya za Mashiriki ya Kati na Afrika Kaskazini kama sehemu ya shughuli zetu za Ramadhani mwaka 2022.
Kwa ushirikiano na SOS Children’s Village nchini Algeria, QNET iliandaa chakula cha jioni cha iftar na kufuatiwa na jioni iliyojaa burudani na vicheko.
Familia mia moja zilizo na changamoto za kifedha nchini Moroko zilipewa muda wa maongezi wa simu, ili waweze kuzungumza na kuungana na familia zao na wapendwa wao, na pia kulipia huduma muhimu wakati wa mwezi mtukufu.
Kwa ushirikiano na SERGAS katika Umoja wa Falme za Kiarabu, QNET iliandaa tukio la mwezi wa Ramadhani mwaka 2022 katika kambi ya SERGAS huko Sharjah. Ikihamasishwa na “Mpango wa Milo Bilioni 1 wa serikali’ ya UAE, QNET ilitoa chakula kwa vibarua 150 pamoja na kuandaa shindano jepesi na la kuburudisha na kupata nafasi ya kujishindia zawadi.
Milo ya iftar pia iliandaliwa kwa jamii zenye uhitaji kote Misri, Kuwait , Saudi Arabia , Qatar na Iraq.
Kuchangamsha Mioyo ya Jamii Barani Asia
Kwa usaidizi wa shirika lisilo la faida la World Human Relief (WHR) lenye makao yake Uturuki, QNET ilitoa chakula muhimu na mboga kwa zaidi ya familia 200 zilizo katika hatari ya kifedha.
Matukio ya Ramadhani ya mwaka 2022 nchini Kazakhstan yalipangwa katika nyumba ya watoto huko Nur-Sultan. Wawakilishi huru wa QNET, wafanyakazi wa ukumbi wa jiji na wafanyakazi wa QNET waliwashangaza watoto na uwanja wa michezo wa nje uliowekwa hivi karibbuni. Watoto pia walipewa safari ya kwenda kwenye ukumbi wa sinema na karamu ya chai.
QNET ilieneza matumaini kwa watoto wa vituo vya kulea watoto yatima vya Muhammadiyah Putat na Baitul Hijarah nchini Indonesia kwa kuwahudumia kwa siku katika viwanja vya michezo vya elimu vya Kidzania Surabaya kwa Ramadhani mwaka 2022.
“Tunaamini kwamba ili mabadiliko yatokee, yanaanza na sisi” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa QNET Malou Caluza. “ Tuna bahati kuwa katika nafasi ya kutoa msaada kw awale wanaohitaji msaada. Tunaamini tunajukumu la kuwasaidia wale ambao wana matatizo kurejea katika hali zao za kawaida au walio katika nafasi hatarishi, kwa sababu ya ukosefu wa usawa wa kimfumo unaochangiwa na janga hili. Tunashukuru kwa fursa hii, haijalishi ni ndogo kiasi gani,kujitoa kwa jamii zetu na kujenga Ramdhani iliyo salama zaidi. “