Tumekuandalia Kalenda ya Kujipenda ya mwezi huu wa Februari mwezi wa upendo ili ufatilie. Hivi ndiyo njia yetu ya kukuonyesha kwamba bidii yako na uaminifu wako haujapita bure bila kutambuliwa. Tunakuthamini na kila kitu unachofanya. Unatokea kila siku bila kujali ugumu wa maisha , haswa baada ya miaka miwili katika janga la kimataifa. Kalenda hii ya Kujipenda ina orodha ya mambo unayoweza kufanya ili kujionyesha upendo kwa niaba yetu.
Kujipenda Ni Nini?
Wakati mwingine, upo na bize sana kutunza wengine na biashara yako kiasi kwamba unasahau kutenga muda kwaajili yako. Kuonyesha kujipenda ni wakati unapoweka kando wakati fulani katika siku yako ili kujipenda, kujitunza na kuzingatia uzima wako, kusikiliza kile ambacho mwili na akili yako inataka, na kujikubali kikamilifu – bila kujali kasoro zako zinazoonekana. Ni kuweka juhudi na upendo uleule kwaajili yako kama unavyo fanya kwa ajili ya familia yako ya QNET na timu yako.
Kalenda ya Kujipenda ya QNET
QNET imeunda kalenda ya shughuli za kuchochea kujipenda. Tunataka iwe zaidi ya vidokezo vya kujitunza ili kukupa baadhi ya vidokezo unavyoweza kufuata ili kutunza afya yako ya akili na kimwili. Unaweza kupakua kalenda hapa, utufuate kwenye akaunti Rasmi za mitandao ya kijamii za QNET au upakue QNET Mobile App ili kupokea taarifa za hapo kwa papo.
“Naahidi Kujipenda” Challenge
Kwa siku 14 zijazo, fuata mawaidha yetu yatakayokusaidia kuepukana na mambo hasi, tenga muda kujithamini, na kuangazia zaidi ukuaji wako binafsi. Je, uko tayari kwa challenge?
Usisahau kushiriki nasi picha na video zako ukitumia moja ya vidokezo vyetu vya Kalenda ya Kujipenda. Mwishoni mwa mwezi huu, QNET itachagua mambo muhimu na kuyashiriki/kusambaza kwenye chaneli zetu rasmi za mitandao ya kijamii. Tunashauku ya kuona unajipenda jinsi tunavyokupenda. Je, uko tayari kufanya ahadi?